Rostam Kaka Tuchati Lyrics

Rostam – Kaka Tuchati Lyrics

Rostam – Kaka Tuchati Lyrics


Oooii naona mtandao unakatika

Upo kimya sana mkato au kunde imevunjika

Na mtanyooka roundi hii

Na hivi huwezi bila mimi?

Najikuta Jay Z oya unarudi lini?

Kaka huku wamefunga mipaka

Ila tiketi nilikata nirudi kabla ya pasaka

Rudi ugeuze kisu sio

Mwana wa kulitafuta mwana wa kulipata

Round hii sio nunio, daraja la mpasu

Kumekucha hivi saa ngapi huko nipe takwimu

Nimeamka nishaweka bundle namngoja Umi mwalimu

Anapambana yule dada

Tanga nimewavulia kofia wametoa sanitizer za iliki

Yaani ukipaka unanukia

Hehehe Corona nishai yaani Bongo kila mtu daktari

Masai kachemsha maji ya mpapai kanywa na sukari

Guza hadi maski wanafua sijui ni nani kawafundisha

Huku kuna dada kajifukiza mashetani kayapandisha

Tueke siasa kando unajua uchumi unashuka

Sio Bongo tu hadi ngambo watu wamefunga maduka

Hapa nawaza pesa ya bango benki walokopa wanajuta

Tukisema tukae ndani na hii njaa si tutakufa

Hali inatisha na umasikini, tunaoumia ni sisi

Yaani bora ufe kwa Ukimwi angalau utaandika urithi

Kwa iyo hamna bata, sio kidimbwi sio tipsi

Kaka madanga yamekata so hazitimbi hizo piece


Bwana wa mabwana Mungu wa miungu

Alpha na Omega nani kama wewe

Bwana wa mabwana Mungu wa miungu

Alpha na Omega nani kama wewe


Hivi unakaa jimbo gani au Marekani

Unajikinga vipi maana vifo vingi hadi siamini (Mmmh)

Au umesharudi ipo zako Horohoro nini

We bwana hebu niache mi nimeze chloroquine

Umenikumbusha kweli Chloroquine ni dawa?

Bado inafanyiwa uchunguzi ila haijadhibitishwa

Ingawa ukinywa haitohatarisha ndio maana bado wanaigawa

Mi ninakunywa maana nilishika uso kabla ya kunawa

Eti unaweza ukawa nayo na usionyeshe dalili?

Ewaah! Uko sahihi, na kingine kuhusu hili ni kwamba

Mgonjwa wa Corona unaweza usimtambue kwa macho

So mtu yeyote unayemuona mpe mita mbili toka kwako

Na hiko kiVansileka ndo kinini baba wawili?

Ni ventilator, ni mashine ka mapafu ya nje ya mwili

Mmmh sijaelewa hebu nieleweshe kuhusu hili

Naskia vinauzwa ghali basi viwe vingi Muhimbili

Okay, kirusi cha Corona kinashambulia mapafu

Ndipo zinaanza homa, kifua alafu

Unashindwa kupumua na mwili unahitaji tafu

Ventilator huingiza hewa na kuitoa iliyo chafu

Tuepuke mikusanyiko ikibidi tukae ndani

Tumeambiwa tujifukize hivi ni dawa unadhani?

Ngoja kwanza, hivi fumigation (Mmmmh mmh)

Baba ile inaua mende eti (Hahaha wacha utani)


 Bwana wa mabwana Mungu wa miungu

Alpha na Omega nani kama wewe

Bwana wa mabwana Mungu wa miungu

Alpha na Omega nani kama wewe


Maisha ya upweke yanasumbua ila siku zinapita

Yule mkewe itunze pete

Mtayamaliza na uhakika kaka

Ila hatua dua haina haja ya kusikitika

Ila navyokujua hujazini miezi sita?

Kiukweli mi mwaminifu ingawa jogoo anawika

Mama Ivan mbabaifu haku-cheat una uhakika?

Kuna mchezaji wa Yanga namwona anapita pita

Nitamkata kata mapanga yaani namuua na namzika

Oyaah wape nyumbani basi pesa ya matumizi

Kaka nitoe wapi na show hakuna siku hizi?

Hali imekuwa ngumu hakuna pesa kila kona

Kila mtu unayemdai naye anasingizia Corona

Mbona sasa wanafunga shule na vyuo alafu bar hawafungi

Mzazi atamlindaja mtoto na akirudi yuko tungi?

Polisi India wanapiga watu wakisongamana

Wao barakoa hawana, jua defender wamebanana

Sasa wanatukusanya kutuambia tusikusanyike

Ila wauguzi wanajitoa sana, dah Mungu awalipe

Wapinzani mnatangaza vifo walopona hamwatangazi

Ah-ah wanasema wangeweka takwimu za wazi ingekuwa kizazi

Kwa hivyo lockdown hakuna alafu umeona text niliyotuma?

Ipi kwenye group mbona inbox hakuna?

Ah naskia (Nini?) koyuzeka mbochi

Maana uliko uliko usiongee sana inatosha

Hadi papai lina Corona dah (Kaka tuchati)

Mmmh ina mbuzi vipi? (Eeh eh kaka tuchati)

Mwili umekufa ngazi (Kaka tuchati)

Poa mwanangu tuendelee kujifukiza

For more:

error:
Open WhatsApp Chat.
1
Say Hi 👋
Hello😊